Maelezo ya Udhuru wa Kufurushwa kwa COVID-19 | Eviction Moratorium - Swahili

Imesasishwa Julai 16, 2020

Mnamo Juni 26, 2020, Bunge la Jimbo la Oregon liliidhinisha HB 4213, inayopanua udhuru wa jimbo zima wa kufurushwa wa miliki za kibiashara na kimakaazi mpaka Septemba 30, 2020. Mswada pia unawapatia wanaoingia upya hadi Machi 31, 2021 ili kulipa kodi zinazodaiwa. 

Pata maelezo zaidi kuhusu udhuru hapo chini.

Je, huwezi kulipa kodi?

Ikiwa wewe ni mpangaji hapa Oregon usiyeweza kulipa kodi yako, huwezi kufurushwa kwa kutolipa wakati wa udhuru. Si lazima utoe ithibati ikiwa huwezi kulipa.

Wapangaji watakuwa na kipindi cha fursa ya kulipa cha miezi misita, ambacho kitadumu kuanzia Oct. 1, 2020 hadi Machi 31, 2021, ili kulipa kodi iliyokusanyika kwenye kipindi cha udhuru. Wakati wa kipindi cha fursa ya kulipa, wapangaji itabidi walipe kodi yao yote ya sasa zinapotakikana, mbali na kodi zozote walizokuwa wanadaiwa.

Ikiwa wewe ni mpangaji

outline of a person with a check next to it

 • Udhuru unalinda yoyote anayeingia tena asiyeweza kulipa kodi asiweze kufurushwa mpaka Sept. 30, 2020.

 • Kusitisha pia kunamlinda mpangaji yeyote dhidi ya kufukuzwa bila sababu hadi Septemba 30, 2020.  

 • Haiwalindi wapangaji wa makazi waliofukuzwa kwa sababu nyingine halali, lakini mwenyenyumba lazima amjulishe mpangaji wake sababu ya kumfukuza.

calendar icon

 • Ikiwa unaweza kulipa kodi unapotakikana, unafaa kulipa kodi.

documents

 • Si lazima utoe ithibati ya kupoteza kipato kwa mwenye nyumba wako.

 • Hata hivyo, hifadhi hati zote, kwa sababu unaweza kustahiki mipango yoyote iwezekanayo ya usaidizi wa kodi ya jimbo au shirikisho.

money sign

 • Kipindi cha fursa ya kulipa kinaanza baada ya udhuru kuondolewa. Utakuwa na kuanzia Oct. 1, 2020 hadi Machi 31, 2021 ili kulipa kodi kwenye kipindi acha udhuru.

 • Wakati wa kipindi cha fursa ya kulipa, itabidi ulipe kodi zako zote za sasa zinapotakikana, mbali na kodi zozote ulizokuwa unadaiwa.

scales of justice

 • Wenyenyumba ambao wanakiuka sehemu yoyote ya sheria hii ya kusitisha kufukuza wanaweza kushtakiwa na mpangaji kwa kiasi cha hadi mara tatu ya kodi ya kila mwezi.

 • Tafuta usaidizi au ushauri wa kisheria kutoka kwa rasilimali za jamii kama vile Muungano wa Jamii ya Wapangaji au Huduma za Msaada wa Kisheria za Oregon ikiwa mwenye nyumba wako anakutishia kukufurusha, anahusisha ada za kulipa kuchelewa, au ikiwa unahitaji mwongozo zaidi.

 • Wenye nyumba na wapangaji wanaoishi kwenye nyumba zao wanaweza kuingia kwenye mpango wa malipo maadamu wahusika wote wawili wako tayari. Hakuna sharti lolote la kisheria linalolazimu uingie kwenye mpango wa malipo.