Ilisasishwa tarehe 15 Aprili, 2021

Maafisa wa afya wa jimbo na serikali wamewaomba watoaji wa chanjo kusitisha kwa muda kutumia chanjo ya Johnson & Johnson. Hatua hii itasaidia kufanya uchunguzi wa visa sita ambapo wanawake wa miaka 18 hadi 48 walipata madhara makali ya kuganda kwa damu. Zaidi ya dozi milioni 6.8 za chanjo ya J & J zimetumika Marekani.

Kwa kawaida watu wanaweza kupata athari kidogo kwa siku chache baada ya kupata chanjo. Hizi ni pamoja na maumivu ya kichwa, joto jingi, au uchovu. 

Ukihisi maumivu makali ya kichwa, maumivu ya tumbo, maumivu ya mguu, au kuishiwa na pumzi ndani ya wiki tatu baada ya chanjo unapaswa kupiga simu kwa 911 au kwenda kwenye chumba cha dharura. Mfahamishe mtoa huduma wako kwamba ulikuwa umepata chanjo ya Johnson and Johnson.

Tutaendelea kuishi na COVID-19 hadi watu wengi watakapopatiwa chanjo au tutakapopata tiba. Kukaa nyumbani kadri iwezekanavyo na kupunguza kutangamana na watu ambao hauishi nao bado ni njia bora zaidi ya kujilinda mwenyewe na jamii. Pia kuhakikisha vituo vyetu vya huduma za afya vinapatikana kwa wale wanaovihitaji.

Kanuni na Mwongozo

Miongozo ya Mfumo wa Afya na Usalama ya Jimbo la Oregon inapendekeza kupunguzwa kwa shughuli kulingana na kiwango cha hatari cha wilaya.

Wilaya ya Multnomah iko katika kategori ya “Hatari Kubwa”, hivyo kuna ukomo wa idadi ya watu wanaoweza kukusanyika na sheria mpya za biashara.

Tafadhali tembelea tovuti ya Gavana kwa taarifa mpya zaidi za sheria na makatazo.

Vizibauso vinahitajika Oregon kwa kila mtu mwenye umri wa miaka 5 au zaidi.

Uangalizi na huduma kwa ajili yako na familia yako

Ikiwa huna daktari, piga simu 211 au Vituo vya Afya vya Msingi vya Wilaya ya Multnomah: 503-988-5558. Wakalimani wanapatikana.

Katika kliniki ya Wilaya ya Multnomah

 • Si lazima uwe na bima ya afya.
 • Si lazima uwe na kipato.
 • Unaweza kupata huduma ya afya bila kujali hali yako ya uhamiaji.
 • Hatutatoa taarifa zako kwa watekelezaji sheria au maafisa wa uhamiaji.

Uhamiaji na Forodha wana sera ya kuzuia ukamataji katika vituo vya huduma za afya, kama vile hospitali, ofisi za daktari, zahanati za afya, na vituo vya huduma za dharura au za haraka. https://www.ice.gov/coronavirus

Ikiwa utapata matibabu au huduma za COVID-19, hakutaathiri ombi lako la makazi ya kudumu Marekani. Soma zaidi kuhusu Wajibu wa Umma.

Je, ninawezaje kupata chanjo ya COVID-19?

Oregon inajitahidi kutoa chanjo kwa kila mmoja kwa awamu. Ikiwa unastahiki kupata chanjo, tumia nyenzo ya kupanga ratiba kwenye tovuti ya Mamlaka ya Afya ya Oregon.

Hivi sasa, hakuna chanjo za kutosha kila mtu ambaye anastahili kupata chanjo. Bado unaweza kusubiri wiki kadhaa ili kupata chanjo, hata kama unastahiki.

Ikiwa uko katika kikundi mojawapo kati ya vile vilivyopewa kipaumbele katika Awamu ya 1A na unahitaji msaada kupanga ratiba kupitia tovuti ya OHA kwa sababu ya lugha au vikwazo vya teknolojia, unaweza kuwasiliana na Wilaya ya Multnomah: 503.988.8939 au covidvaccineinfo@multco.us. Tunaweza kukusaidia kujaza fomu ya mtandaoni. Simu na barua pepe tunazopokea ni nyingi sana. Tunatoa kipaumbele kwa simu kutoka kwa wale walio katika Awamu ya 1A wenye vikwazo vya kupata tovuti ya OHA.

Taarifa Zaidi za Chanjo

How the COVID Vaccines Protect You - Swahili (623.65 KB)

After you get vaccinated for COVID-19 - Swahili (486.07 KB)

Njia bora ya kupata taarifa kuhusu chanjo ya COVID-19 katika Wilaya ya Oregon ni kutembelea tovuti ya chanjo ya OHA COVID-19.

Pia unaweza:

 • Tuma neno ORCOVID kwenda 898211 ili upate taarifa mpya ujumbe mfupi wa simu/Arafa (Kiingereza na Kihispania pekee)
 • Barua pepe ORCOVID@211info.org (Lugha zote)
 • Piga Simu Kituo cha Kupiga Simu kwa 211 au 1-866-698-6155 (TTY: Piga simu 711 na piga simu 1-866-698-6155). Iko wazi 12 alfajiri-1 usiku kila siku, kiwemo siku kuu.

Je, nani anapaswa kupimwa COVID-19?

Unapaswa kupimwa ikiwa una dalili za COVID-19 au ikiwa ulitangamana kwa karibu na mtu mwenye COVID-19. Utangamano wa karibu unamaanisha kuwa ndani ya umbali wa miguu 6 kutoka kwa mtu mwingine kwa dakika 15 au zaidi , ukiwa na au bila barakoa.

Upimaji COVID-19 »

Sherehe na Mikusanyiko ya Msimu

Hakuna mkusanyiko ambao hauna hatari. Kukaa na watu wachache kwa muda mfupi ni salama zaidi.

Zingatia vidokezo hivi vya njia za kusherehekea sikukuu na tamaduni kwa usalama zaidi (CDC) »

Unaweza kupunguza hatari yako ya kupata au kueneza COVID-19:

 • Fanya kidogo
 • Fanya kifupi
 • Fanya nje

Dumisha umbali wa mtu na mtu wa angalau miguu sita na kuvaa kifunikauso.

Zuia Kuenea kwa COVID-19

Watu wenye matatizo mengine ya kiafya, kama vile pumu, ugonjwa wa kisukari, au moyo au mapafu, wako katika hatari kubwa ya kuugua sana COVID-19. 

Virusi ambavyo husababisha COVID-19 huenea kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Ili kuepuka kuugua:

 • Nawa mikono yako mara kwa mara
 • Vaa barakoa unapotoka nje
 • Epuka kugusa uso wako
 • Ziba mdomo unapokohoa au unapopiga chafya
 • Kaa angalau miguu 6 kutoka kwa watu ambao hauishi nao
 • Hakikisha mikusanyiko inakua midogo, mifupi, na inafanyika nje wakati wowote kadri inapowezekana
 • Safisha na kuua vimelea katika maeneo yanayoguswa sana
 • Punguza safari na ukae karibu na nyumbani

Ikiwa unajisikia kuumwa

Ukianza kuhisi kuumwa - hasa homa na kikohozi:

 • Kaa nyumbani na mbali na watu wengine.
 • Mpigie simu daktari wako au kliniki ili uone ikiwa unahitaji kupimwa.
 • Kaa nyumbani hadi daktari au kliniki yako itakaposema unaweza kuwa karibu na watu wengine tena.
 • Fanya vitu ambavyo kwa kawaida hufanya ili ujisikie vizuri: lala, pumzika, kunywa maji mengi.

Hakuna dawa maalum ya COVID-19.

Tafuta huduma ya afya ya dharura mara moja ikiwa wewe au mtu yeyote wa umri wowote anaonyesha dalili hizi za dharura:

 • Kupumua kwa shida
 • Maumivu ya kudumu au shinikizo kwenye kifua
 • Mkanganyiko mpya
 • Kushindwa kuamka au kukaa macho
 • Midomo au uso wa hudhurungi
 • Maumivu makali ya tumbo

Piga simu 911 au piga simu kwenye kituo cha dharura cha mahali ulipo. Mwambie mhudumu kwamba wewe au mtu anayehitaji msaada anaweza kuwa na COVID-19

Nyenzo

Karatasi ya maelezo ya COVID-19 Community Flyer

CAWEM na COVID19

Kituo cha Huduma za Mawasiliano cha Afya ya Akili cha Multnomah | 503-988-4888, bila malipo 800-716-9769 - Usaidizi wa bure saa 24 kila siku, na wakalimani wanapatikana.

Maswali?

Piga simu 2-1-1, siku 7 kwa wiki kuanzia saa 2 asubuhi hadi 5 usiku| au tembelea 211Info