drive-up COVID-19 testing at East County Health Center

Ilisasishwa tarehe 11 Januari, 2021

Upimaji wa COVID-19

Unapaswa kupimwa ikiwa una dalili za COVID-19 au ikiwa ulitangamana kwa karibu na mtu mwenye COVID-19. Kutangamana kwa karibu kunamaanisha kuwa karibu na mtu ndani ya umbali miguu 6 kwa dakika 15 au zaidi katika siku, ukiwa na au bila barakoa.

Ikiwa unapimwa kwa sababu ulitangamana kwa karibu na mtu ambaye ana COVID-19, ni bora ukisubiri angalau siku 4 baada ya kutangamana na kabla ya kupimwa. Upimaji hautakuwa na maana ikiwa utafanyika muda mfupi baada ya kutangamana. Unapaswa kukaa nyumbani na mbali na watu wengine wakati unaposubiri.

Unaweza kupimwa katika ofisi ya daktari wako au kliniki. Ikiwa huna daktari, unaweza kupimwa kwenye eneo la kupimwa la jamii.

Maeneo ya Kupima ya Jamii

Upimaji wa bila malipo unapatikana kwa miadi kwa mtu yeyote mwenye dalili au mtu yeyote ambaye ametangamana kwa karibu na mtu mwenye COVID-19. 

Piga simu 503-988-8939 kwa ajili ya miadi au kwa taarifa zaidi. Kuna wakalimani.

Maeneo ya Kupimwa na Muda

Muda au sehemu ya kituo cha upimaji inaweza kubadilishwa, na vituo vipya vinaweza kuongezwa. Piga simu kwa taarifa mpya.

Upimaji wa Jamii katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Mashariki - Maegesho
600 NE 8th St, Gresham
Jumatatu na Alhamisi, saa 3:00 asubuhi - saa 9:45 alasiri

PCC Cascade Campus - Ushirikiano wa REACH
705 N Killingsworth St, Portland
Jumatatu na Alhamisi, saa 3:00 asubuhi - saa 9:45 alasiri

Mid County Community Testing - IRCO
10301 NE Glisan St. Portland
Ijumaa, saa 6:00 mchana - saa 12:00 jioni

Rockwood Community Testing - Mtandao wa Latino
312 SE 165th Ave. Portland
Jumamosi, saa 3:00 asubuhi - saa 9:45 alasiri

Upimaji, hali ya uhamiaji na malipo ya umma 

  • Si lazima uwe mkazi wa Wilaya ya Multnomah au uwe na bima ya afya ili uweze kupimwa katika vituo vyetu vya jamii.
  • Unaweza kupimwa bila kujali hali yako ya uhamiaji. 
  • Hatutoi taarifa zako kwa watekelezaji sheria au maafisa wa uhamiaji.

Uhamiaji na Forodha wana sera inayozuia ukamataji katika vituo vya huduma ya afya, kama vile hospitali, ofisi za daktari, kliniki za afya, na vituo vya huduma za dharura au za haraka.

Ikiwa unapata matibabu au huduma za COVID-19, hakuwezi kukuathiri wakati unapoomba makazi ya kudumu Marekani. Soma zaidi kuhusu Wajibu wa Umma.

Vituo vya Upimaji vya OHSU

Piga simu 833-647-8222 au tembelea tovuti ya OHSU kujua vituo na taarifa zaidi. 

Baada ya kupimwa

Ukigundulika kuwa na virusi

Hatua ya 1: Kaa nyumbani na mbali na watu wengine, hata watu ambao unaishi nao. Ikiwa una dalili, unaweza kuwa karibu na watu wengine baada ya:

  • Kupona homa kwa saa 24 bila kutumia dawa, NA
  • Dalili zako kupungua, NA
  • Angalau siku 10 zimepita tangu ulipokuwa na siku ya kwanza ulipokuwa na dalili

Ikiwa huna dalili , unaweza kutangamana na watu wengine baada ya:

  • Siku 10 kupita tangu upimwe, na kutokuwa na dalili

Watu ambao unaishi nao wanapaswa pia kukaa nyumbani na mbali na watu wengine nje ya kaya yako kwa siku 14. Kwa maswali kuhusiana na jambo lolote kati haya, mpigie simu daktari wako.

Hatua ya 2: Waambie watu uliotangamana nao kwa karibu mara moja kwamba umegundulika kuwa na maambukizi. “Kutangamana kwa karibu" kunamaanisha umekuwa karibu na mtu mwingine kwa dakika 15 katika siku, na au bila barakoa. Waambie wanapaswa kukaa nyumbani kwa siku 14 tangu mara ya mwisho walipokuwa karibu na wewe na kupata kipimo cha COVID-19, hata kama hawana dalili.

  • Ikiwa una dalili: wasiliana na watu ambao ulikuwa umetangamana nao kuanzia siku 2 kabla ya dalili zako kuanza.
  • Ikiwa huna dalili: wasiliana na watu ambao ulikuwa umetangamana nao kwa karibu kuanzia siku 2 kabla ya kupimwa COVID-19. 

Hatua ya 3: Pata usaidizi ikiwa unahitaji. Piga simu 2-1-1 ikiwa unahitaji msaada kwa kujitenga au kujiweka karantini. Wanaweza kukusaidia kupata nyenzo unazohitaji (bidhaa za chakula, msaada wa kifedha, msaada wa kodii, vitu vingine muhimu). 

Mfanyakazi wa afya ya umma anaweza kukupigia simu. Wanaweza pia kukusaidia kuwasiliana na watu ambao ulitangamana nao kwa karibu ikiwa unahitaji msaada. Tafadhali pokea simu yao. Hawatatoa taarifa zako kwa uhamiaji au watekelezaji wa sheria.

Iwapo hujakutwa na maambukizi ya COVID-19

Ikiwa ulikuwa karibu na mtu mwenye COVID-19, endelea kukaa nyumbani hadi  siku 14 zipite tangu ulipotangamana naye - hii inaitwa karantini. Kukaa nyumbani na mbali na watu wengine ambao hauishi nao kwa siku 14 ndiyo njia salama zaidi ya kuzuia kueneza COVID-19 kwa wengine.

Ikiwa huna dalili, na hufanyi kazi au kukaa katika mazingira ya makazi ya watu wengi - kama vile kituo cha uangalizi wa muda mrefu - unaweza kumaliza karantini baada ya siku 10. Ikiwa unaishi na mtu aliye katika hatari ya kuumwa sana, kaa karantini kwa siku 14 kamili. Mpigie simu daktari wako ikiwa una dalili yoyote.

Endelea kujilinda na kuwalinda wengine: vaa barakoa, kaa umbali wa miguu 6 kuroka kwa wengine, nawa mikono yako mara kwa mara.