gramma and grandaughter together washing handsWengi wetu tunaishi na familia, marafiki, au wakazi wenza katika nyumba moja, au pamoja na watoto, babu/bibi na wazazi.

Watu wenye umri wa miaka zaidi ya 65, au mtu yeyote mwenye ugonjwa wa mapafu, shinikizo la juu la damu, pumu, kisukari wapo hatarini ya kuugua zaidi kutokana na COVID-19. Ikiwa mtu mmoja nyumbani yuko hatarini, kila mmoja anapaswa kuchukua tahadhari zaidi za kujizuia kuugua ili kumlinda.

Hapa ni baadhi ya vidokezo vya jinsi tunaweza kuishi salama, pamoja.

Hatua za kuchukua kila siku

Nawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji kwa angalau sekunde 20.

 • Hakikisha umenawa mikono unaporudi nyumbani, kabla ya kula, baada ya usafi, au baada ya kutoka bafuni.
 • Familia zinaweza kubadili unawaji mikono kuwa mchezo kwa kuimba wimbo wa sekunde 20 kwa pamoja wanapo nawa mikono.

Usiguse macho, pua, au mdomo wako kwa mikono ambayo haijaoshwa.

Tumia karatasi ya shashi unapokohoa au kupiga chafya, au tumia ndani ya kiwiko chako. Tupa karatasi za shashi zilizotumika kisha unawe mikono yako. 

Safisha na utumie vipukusi kuua vijidudu katika nyuso zinazoguswa mara kwa mara kama vile meza, viti, vitasa vya milango, swichi za taa, rimoti, vidude vya kuchezea watoto, vyoo, na makaro mara kwa mara. Ikiwezekana, tumia glavu za kutupwa baada ya matumizi/au nawa mikono baada ya kusafisha nyuso hizo.

Unapofua, tumia maji moto na kausha vifaa kabisa. 

 • Usitikise nguo chafu 
 • Nawa mikono baada ya kuzishika nguo chafu

Panga kwa ajili ya afya ya kila mtu

 • Weka mpango wa namna utakavyohudumiwa ikiwa utaugua. Wafahamishe mnaoishi nao katika kaya kuhusu mpango huo. Jumuisha jina na nambari ya simu ya daktari au kliniki chako. Jumuisha taarifa kuhusu tatizo lolote la afya linaloendelea kama vile pumu au kisukari ikiwemo matibabu ambayo unapaswa kupata. 
 • Weka mpango kwa yule atakayewahudumia watoto wako na wengine katika kaya yako wanaohitaji usimamizi au uangalizi.
 • Ikiwa una matatizo yanayoendela ya kiafya (hali zilizokuwapo) ambayo yanakuweka katika hatari kubwa ya kuugua sana, hakikisha unapata dawa na vifaa vya kutosha iwapo unahitaji kukaa nyumbani kwa wiki chache.

young men making dinner togetherIkiwa unafanya kazi nje ya nyumba yako

Ili kulinda afya ya kila mtu: 

 • Badilisha nguo na viatu vyako unapofika nyumbani. Kisha nawa mikono yako kwa angalau sekunde 20. 
 • Kama unaweza, kaa umbali wa futi 6 kutoka kwa watu wengine ndani ya nyumba yako.
 • Hakikisha kila mtu anavaa barakoa za uso kama haiwezekani kukaa umbali wa futi 6.

Ikiwa mmoja wenu ataugua

 • Jaribu kutenga nafasi tofauti kwa mtu huyo kukaa hadi apone.
 • Ikiwezekana, mpatie mgonjwa bafu atakayoitumia pekee yake.
 • Ikiwa kuna bafu moja tu, hakikisha inasafishwa kila mara baada ya kutumiwa na mtu anayeugua.
 • Usitumie taulo, malazi, chakula, barakoa za uso au vyombo na mtu mwingine.
 • Mchague mtu mmoja aliye na afya nzuri katika kaya kumtunza mgonjwa.
 • Vaa barakoa ya uso unapomtunza mgonjwa. 
 • Ikiwezekana, pia mgonjwa anapaswa kuvaa barakoa ya uso, ili kuwalinda wengine anaoishi nao.